Henock, Kapombe, Mzamiru waingia kinyang’anyiro mchezaji bora Februari

Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kuwania mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Februari (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao ni mlinzi wa kati Henock Inonga, mlinzi wa kulia Shomari Kapombe na kiungo mkabaji Mzamiru Yassin.

Nyota wengine Mohamed Hussein na Sadio Kanoute wameingia katika tano bora lakini baada ya mchujo wamebaki watatu.

Katika mwezi Februari tumecheza mechi tano, tatu zikiwa za Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili za Ligi Kuu ya NBC huku nyota hao wakicheza zote.

Takwimu za wachezaji wote za Februari

Dakika Mechi Magoli Assist

Henock 450 5 1 0

Kapombe 450 5 0 1

Mzamiru 450 5 0 0

Zoezi la kupiga kura linaanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Machi mosi saa sita mchana.

Mshindi atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER