Mlinzi wa kati Henock Inonga Baka raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amejiunga na kikosi chetu kutoka DC Motema Pembe.
Baka maarufu Varane tayari amejiunga na kikosi chetu kinachoendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22 hapa nchini Morocco.
Kabla ya kujiunga nasi Varane 27,
alikuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Motema Pembe pamoja na timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Varane anaungana na Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Ibrahim Ame kujenga ukuta imara wa timu yetu katika idara ya ulinzi wa kati.
Varane anakuwa mchezaji wa tano kujiunga nasi msimu huu baada ya Peter Banda, Yusuph Mhilu, Duncan Nyoni na Pape Ousmane Sakho
One Response
Sajili nzuri ya kuleta kijana pale kuongeza kasi kwenye kukaba