Hawa hapa nyota watakaotuwakilisha dhidi ya Mbeya City

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka kwenye Uwanja wa Sokoine kuikabili Mbeya City katika mtanange wa Ligi Kuu ya NBC ambao tunaamini utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuukabili.

Katika mchezo huo, Kocha Mkuu Pablo Franco, ameamua kuanza na viungo watatu wa ulinzi kutokana na aina ya mchezo wa wapinzani pamoja na jinsi uwanja ulivyo.

Kocha Pablo amewaanzisha kwa pamoja Jonas Mkude, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin ili kuimarisha eneo letu la kiungo na kuanzisha mashambulizi.

Chris Mugalu ataongoza mashambulizi akipata msaada wa karibu kutoka kwa Kibu Denis na Bernard Morrison.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Mzamiru Yassin (19), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Kibu Denis (38), Bernard Morrison (3)

Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Hassan Dilunga (24), Pape Sakho (10), Medie Kagere (14), John Bocco (22), Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER