Hatutaingia kinyonge kwa Mkapa Jumapili

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amewahakikishia mashabiki katika mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi tutacheza kwa mamlaka yote kama tunavyofanya tukiwa Benjamin Mkapa.

Ahmed ameyasema hayo wakati akizunguka mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam kuanzia Tawi la Mpira Pesa lililopo Magomeni Mikumi, Soko la Magomeni, Manzese mpaka Mabibo Sokoni kwa ajili ya hamasa, kuuza tiketi na jezi.

Ahmed amesema mashabiki waje kwa wingi Jumapili wakiwa na uhakika wa kushuhudia kandanda safi kutoka kwa vijana wa Kocha Juma Mgunda.

“Tukiwa nyumbani hatuingii kizembe, lazima wapinzani wajue kwamba wamefika Tanzania, wapo nyumbani kwa Mnyama. Tutafanya balaa kubwa zaidi, Hatujamalizaaaa,” amesema Ahmed Ally.

Tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa nchini Malawi Jumamosi iliyopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER