Hatukufanikiwa kutinga nusu fainali ya AFL

Sare ya kufungana bao moja ugenini dhidi ya Al Ahly haijaweza kutusaidia kutinga nusu ya African Football League (AFL) kutokana wa wapinzani wetu kunufaika na bao la ugenini.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa tulitoka sare ya mabao 2-2 hivyo Al Ahly wamesonga kwa faida ya bao la ugenini.

Tulianza mchezo taratibu huku tukiwasoma Al Ahly ambao walimiliki sehemu kubwa katika dakika 30 za mwanzo.

Sadio Kanoute alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 68 akimalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Clatous Chama aliyemalizia krosi ya Shomari Kapombe.

Mahmoud Kahraba aliisawazishia Al Ahly bao hilo dakika ya 76 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ali Maaloul.

X1: Ally, Kapombe (Phiri 89′), Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Chama (Kennedy 73′), Kanoute, Bocco (Baleke 45′), Ntibazonkiza (Miquissone 80′), Kibu (Onana 80′)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER