Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri, Corneille Hategekimana raia wa Rwanda kuwa kocha mpya wa viungo kwa mkataba wa miaka miwili.
Hategekimana (47) amejiunga nasi akitokea AS Kigali ya nchini kwao Rwanda.
Hategekimana amefuzu mafunzo ya kozi mbalimbali za viungo kwa wachezaji, ana Diploma ya Uongozi wa Michezo, Mkufunzi wa viwango (GPS) kwa wachezaji, Kozi ya juu ya Viungo inayotolewa na FIFA aliyopata Oktoba 2018 Johannesburg, Afrika Kusini.
Wasifu wa Hategekimana kabla ya kutua kwetu…
๐ธAgosti 2022 hadi sasa, Kocha wa Viungo AS Kigali, ambapo ameshinda taji la Super Cup.
๐ธ2021-2022 Kocha wa Viungo Polisi Rwanda.
๐ธ2021 Kocha wa Viungo wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Rwanda.
๐ธ2019-2021 Kocha wa Viungo wa AS Kigali.
๐ธ2018 Kocha wa Viungo wa timu ya Taifa ya Rwanda chini ya umri wa miaka 23.
๐ธ2017-2018 Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha wa Viungo wa Rayon Sports, na ameshinda taji la Ligi pamoja na kufika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
๐ธ2016-2017 Kocha wa Viungo ISONGA Academy FC.
๐ธ2015 mpaka sasa ni Mkufunzi wa CAF katika Sayansi ya Viungo.
๐ธ2007-2017 Mwalimu wa Viungo IFAK Secondary School.
๐ธ 2009-2018 Mkurugenzi wa Ufundi katika Shule ya Gasabo.
๐ธ2014-2015 Kocha wa Viungo wa Kiyovu FC.