Haikuwa bahati yetu

Kikosi chetu kimepoteza kwa bao moja dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni kiashiria cha kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Msimu wa 2021/22.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kadiri huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini mpira ukichezwa zaidi sehemu ya katikati ya uwanja.

Yanga walipata bao mapema dakika ya 12 kupitia kwa Fiston Mayele baada ya kupokea pasi kutoka kwa Farid Mussa.

Mlinzi wa kati Joash Onyango alishindwa kuendelea mpira na kutolewa dakika ya 26 baada ya kuumia kichwani wakati akijaribu kufunga nafasi yake ikachukuliwa na Kennedy Juma.

Kipindi cha pili tulianza kwa kasi na kuliandama lango lango la Yanga ambapo dakika ya 49 Chris Mugalu alipoteza nafasi ya kufunga.

Dakika ya 91 kiungo Taddeo Lwanga alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumfanyia madhambi Feisal Salum.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Hassan Dilunga, Pape Sakho, Sadio Kanoute na Mohamed Hussein kuwaingiza John Bocco, Peter Banda, Mzamiru Yassin na Israel Patrick.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER