Gomez: Tunataka kuonyesha tulistahili kuwa vinara

Licha ya kukiri mchezo wa kesho ambao ni wa mwisho katika hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakuwa mgumu, Kocha Mkuu, Didier Gomez amesema tunahitaji kuonyesha kiwango bora ili kudhihirisha uwezo wetu.

Kocha Gomez amesema tumemaliza tukiwa vinara wa kundi A na tunapaswa kuwa bora zaidi ili kuonyesha Simba imeendelea kukua katika soka la Afrika.

Amesema itakuwa ni heshima kubwa kumaliza hatua ya makundi bila kupoteza mchezo ndiyo maana tunapaswa kuonyesha kiwango kikubwa.

“Tuna mchezo mgumu wa kucheza na pia muhimu kwetu kuwaonyesha kuwa tumekua timu kubwa Afrika na kwa uhakika tumestahili kumaliza nafasi ya kwanza kwenye hili kundi,” amesema Gomez.

Kwa upande wake mshambuliaji kinara Medie Kagere amesema tunaenda kukutana na timu bora lakini nasi tuko vizuri ndiyo maana tumefika hatua hii na tumejipanga kuwakabili.

“Tuna timu nzuri na tunakutana na timu nzuri pia lakini lazima kujua kwamba hii ni Ligi ya Mabingwa ambayo inahusisha mabingwa wa mataifa.

“Kwa upande wetu tumejiandaa kuhakikisha tunaendelea kupata ushindi,” amesema Kagere.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Happy me ☺️
    I will very happy if we grab a draw or a goalless. We improved, yes, but today’s results will elevate Simba Sports Club to Final and win πŸ†πŸ”πŸ¦

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER