Gomez: Tulistahili kushinda lakini huu ndio mpira

Kocha Mkuu, Didier Gomez amesema kwenye mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons tulistahili kupata ushindi lakini mpira una matokeo matatu na ameyakubali.

Gomez amesema tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga na penati pia tulipata lakini hatukuweza kuzitumia kitu ambacho tunapaswa kukifanyia kazi haraka.

Licha ya kucheza mechi kila baada ya siku tatu au nne lakini kocha Gomez amesema hiyo sio sababu ya kupelekea kupata sare hiyo.

“Sijaridhishwa na matokeo, tulikuwa nafasi ya kupata ushindi, tumepoteza nafasi nyingi pia tulikosa mkwaju wa penati lakini ndio mpira.

“Tunapaswa kurejesha hali ya kujiamini na kushinda mechi zijazo, kitu kizuri kwetu ni kuwa bado tuna mechi tatu mkononi ambazo tukifanya vizuri tutakaa kileleni mwa msimamo,” amesema kocha Gomez.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER