Gomez: Mashabiki wa Simba kiboko

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomez, amesema katika nchi zote alizofundisha soka barani Afrika, hajawahi kukutana na washabiki wanaofanana na Wekundu wa Msimbazi.

Akizungumza jijini Arusha mwishoni mwa wiki, Gomez amesema hazungumzi maneno hayo kwa sababu ni Kocha wa Simba lakini bali huo ndiyo ukweli anaouona.

Gomez ameanza kufundisha soka barani Afrika mwaka 2012 akianza katika Klabu ya Rayon lakini amefundisha pia katika nchi za Cameroon, Algeria, Ethiopia na Sudan.

“Mashabiki wa Simba ni wa aina yake. Mimi nimefundisha timu katika maeneo tofauti ya Afrika lakini mashabiki wa Simba ni daraja lingine. Ni vichaa halisi wa soka na mapenzi yao kwa timu yao si ya kawaida,” amesema.

Gomez amesema alishangazwa na umati uliokuwa ukijitokeza mikoani ambako Simba ilikuwa ikicheza na kutoa mifano ya mechi za Lunyasi za Kombe la Shirikisho zilizochezwa Ruvuma na Kigoma alizosema hazikuwa za kawaida.

Aidha, Gomez amesema ndiyo sababu mechi Simba iliyofungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania ilimuumiza zaidi kuliko hata ile waliyofungwa na magoli 4-0 na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

“Kwa washabiki wa soka, pambano la watani wa jadi lina maana ya pekee. Nilijua maumivu ya washabiki wetu wakati ule na hadi leo bado nina kidonda. Sijui hata ilikuwaje Simba ikafungwa katika mechi ile,” amesema.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER