Gomez: Macho yote sasa Ligi Kuu

Muda mfupi baada ya timu kurejea nchini kutoka Misri ilipokuwa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana dhidi ya Al Ahly Kocha Mkuu, Didier Gomez amesema sasa anaelekeza nguvu kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

Kocha Gomez amesema tunahitaji kushiriki Klabu Bingwa kila mwaka hivyo tunapaswa kushinda kila mchezo wa Ligi ili kutetea ubingwa na kupata nafasi ya kurudi Afrika mwakani.

Gomez ameongeza kuwa kwa sasa anaitazama michezo minne ya Ligi iliyopo kwenye ratiba ya mwezi huu na malengo ni kuhakikisha tunashinda yote ili kupanda kwenye msimamo.

Baada ya wachezaji kufika Dar es Salaam mchana huu wameruhusiwa kwenda nyumbani kuziona familia zao na kesho jioni watarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Baada ya kumaliza mechi za makundi za Afrika sasa tunaelekeza nguvu katika Ligi, tunahitaji kucheza Klabu Bingwa kila mwaka na tiketi pekee ni kutetea ubingwa. Tuna mechi nne ndani ya mwezi huu ambazo tunahitaji kushinda ili kukaa kileleni mwa msimamo,” amesema Kocha Gomez.

Akizungumzia mchezo wa jana Gomez amesema amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wetu ingawa hakutaka mechi iishe kwa kupoteza.

“Nimefurahishwa na kiwango chetu cha uchezaji, wachezaji walijituma na kufuata maelekezo lakini sisi ni Simba sikupenda mchezo kumalizika kwa kufungwa,” amesema Gomez.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER