Gomez: Hatuwadharau lakini hatuwaogopi Kaizer Chiefs

Zikiwa zimebaki saa chache kuelekea mchezo wetu wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa uwanja wa FNB Kocha Didier Gomes amesema hatutawadharau wapinzani lakini hatuwaogopi.

Gomes amesema tunatarajia mchezo mgumu kutoka kwa Kaizer kutokana na kucheza ugenini lakini hilo halitaturudisha nyuma kushindwa kutimiza malengo yetu ya kufanya vizuri.

Amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea mchezo na matarajio ya kupata ushindi ni makubwa.

“Hii ni Ligi ya Mabingwa, tunatarajia mchezo mgumu sababu tupo ugenini lakini hatutaki kuzuiliwa. Kaizer ni timu kubwa hatuwezi kuidharau lakini tupo tayari kupambana,” amesema Gomes.

Kwa upande wake Nahodha John Bocco amewataka wapenzi wa Simba kuendelea kuwaombea huku akiahidi kupambana hadi dakika ya mwisho kutafuta ushindi.

“Tuko tayari kuipambania timu yetu na kupata matokeo mazuri, mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kushinda,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER