Gomez: Bado hatujamaliza kazi Klabu Bingwa Afrika

Licha ya kufikisha alama 10 na kuongoza Kundi A katika msimamo wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, baada ya kuifunga El Merrikh mabao 3-0 jana, Kocha Mkuu, Didier Gomez amesema bado hatujamaliza kazi ya kufuzu michuano hiyo.

Licha ya matokeo ya mchezo wa jana sasa tunahitaji alama moja ili kufuzu hatua ya robo fainali ambapo Kocha Gomez amesema bado tunapaswa kupambana kuhakikisha tunapata ushindi kwenye michezo miwili iliyobaki.

Kocha Gomez amewamwagia sifa wachezaji wake kutokana na uwezo mkubwa wanaouonyesha uwanjani licha ya kucheza mechi mfululizo kitu ambacho kinampa faraja.

“Nafurahishwa na viwango vya wachezaji wangu, tunacheza mechi nyingi mfululizo lakini wanapambana na tunapata ushindi hicho ni kitu kikubwa,” amesema Kocha Gomez.

Akizungumzia mchezo ujao wa Klabu Bingwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa Aprili 2, (wapi?) Kocha Gomez amesema anaamini utakuwa mgumu na tunapaswa kujipanga vizuri kabla ya kuwakabili.

“Mchezo wa Vita utakuwa mgumu, Vita wana timu nzuri wanacheza soka la kasi hivyo tunapaswa kujiandaa vema kabla ya kuwakabili,” amesema Kocha Gomez.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER