Kocha Mkuu, Didier Gomez amefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi cha kwanza kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC utakaofanyika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
Gomez amemuanzisha benchi kiungo mshambuliaji Luis Miquissone ambaye amekuwa akianza katika kila mchezo kutokana ubora alionao huku Perfect Chikwende akichukua nafasi yake.
Kocha huyo leo amempunzisha kiungo Taddeo Lwanga ambapo eneo la kiungo wa ulinzi litakuwa chini ya Erasto Nyoni na Jonas Mkude.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein ©
4. Joash Onyango
5. Pascal Wawa
6. Erasto Nyoni
7. Clatous Chama
8. Jonas Mkude
9. Medie Kagere
10. Rally Bwalya
11. Perfect Chikwende
Wachezaji wa Akiba
GK. Beno Kakolanya
02. Kennedy Juma
03. Mzamiru Yassin
04. Bernard Morrison
05. Chris Mugalu
06. John Bocco
07. Luis Miquissone