Gomes:Tumepata somo msimu ujao hatutashikika

Baada ya kushindwa kufuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs, Kocha Mkuu Didier Gomes amesema tumepata somo na msimu ujao tutakuwa bora zaidi.

Gomes amesema kupoteza kwa idadi ya mabao 4-0 katika mchezo wa mzunguko kwanza umetupa kazi kubwa ya kupindua matokeo ambayo si rahisi hasa kwenye hatua hii.

Mfaransa huyo ameongeza kuwa katika mchezo wa kwanza uliopigwa Afrika Kusini wiki iliyopita hatukuwa wazuri kwenye kuzuia na kusababisha kuruhusu idadi kubwa ya mabao kitu ambacho kimetupa somo na msimu ujao tukishiriki haitajirudia.

“Tulikuwa na malengo ya kutinga nusu fainali lakini imeshindikana. Tumejifunza na tukipata nafasi ya kushiriki msimu ujao tutakuwa bora zaidi,” amesema Gomes.

Gomes amewasifu wachezaji wetu kwa kupambana muda wote na kujitoa kwa ajili ya timu katika mchezo wa jana kitu ambacho kinamfanya kujivunia kufanya nao kazi.

“Wachezaji walipambana kwa ajili ya timu, walifanya kila kitu kwa ajili ya timu lakini bahati haikuwa upande wetu kwa kweli najivunia kufanya nao kazi,” amesema Gomes.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER