Gomes: Wachezaji wapo tayari kuweka rekodi Afrika

Licha ya kuwa na kazi kubwa ya kupindua matokeo ya mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs kesho, wachezaji wetu wamejiandaa kufanya majaabu na kuweka historia.

Kauli hiyo imetolewa na Kocha Didier Gomes katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anataka kuwepo kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani.

Gomes amesema kwenye mpira kila kitu kinawezekana na tumejitahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita na kama tukipambana kiume tunaweza kupindua matokeo na kutinga nusu fainali.

“Tunajua tuna kazi kubwa ya kufanya, lakini kwenye mpira kila kitu kinawezekana. Wachezaji wapo kwenye hali nzuri na kila mmoja anatamani ajumuishwe kikosini lengo ni kupindua matokeo na kuweka rekodi barani Afrika.

“Hatuwadharau Kaizer Chiefs, lakini tupo tayari kupambana kiume kuhakikisha tunashinda na kutinga nusu fainali,” amesema Gomes.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Pingback: URL

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER