Kocha Mkuu, Didier Gomes amesesema mchezo ujao wa ligi dhidi ya watani wa jadi Yanga utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Julai 3 utakuwa kama fainali kutokana na umuhimu wake.
Gomes amesema tunahitaji alama tatu pekee ili kutawazwa mabingwa na mechi inayofuata ni dhidi ya watani hivyo anaamini utakuwa mchezo mgumu kama ilivyo fainali.
Gomes raia wa Ufaransa ameongeza kuwa kwa sasa kikosi chetu kipo katika hali nzuri ndiyo maana tumeshinda mechi nyingi mfululizo na anaamini itakuwa hivyo hadi mwisho wa msimu.
“Tumebakisha mechi tano na tunahitaji alama tatu tutangazwe mabingwa na mchezo unaofuata ni dhidi ya watani wetu Yanga najua itakuwa kama fainali, nawaamini wachezaji wangu na tutafanya vizuri na kuibuka washindi,” amesesema Kocha Gomes.
Kocha Gomes hakuacha kuwamwagia sifa wachezaji wetu kutokana na viwango wanavyoonyesha na kudhihirisha kuwa tunastahili kuwa mabingwa kwa mara ya nne mfululizo.