Da Rosa: Mechi na Al Merreikh ni ngumu

Kocha Mkuu, Didier Gomez Da Rosa, amekiri kuwa mchezo wa Klabu Afrika dhidi ya Al Merreikh utakaopigwa wikiendi ijayo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani hao kupoteza mechi mbili za mwanzo.

Da Rosa ambaye alikuwa kocha Al Merreikh kabla ya kujiunga nasi amesema anaifahamu vizuri timu hiyo na anajua haitakuwa rahisi kupoteza mechi ya tatu mfululizo.

“Mechi itakuwa ngumu Al Merreikh wamepoteza mechi mbili mfululizo hawatapenda kupoteza tena ndiyi maana nasema utakuwa mchezo mgumu.

“Nawajua vizuri Merreikh wana wanachezaji wazuri na wanacheza soka safi ingawa nasi ni bora na kama wachezaji wangu wakifuata maelekezo tunaweza kupata ushindi,” amesema Da Rosa.

Simba ndiyo kinara wa kundi A tukiwa na alama sita baada ya kushinda mechi zetu mbili dhidi ya AS Vita na Al Ahly.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER