Gomes, Chama wakabidhiwa tuzo zao za VPL

Kocha Didier Gomes amekabidhiwa tuzo yake ya Kocha Bora wa Aprili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na kiungo Clatous Chama aliyekuwa mchezaji bora wa mwezi huo.

Gomes ameshinda tuzo hiyo baada ya kutuwezesha kushinda mechi zote saba ndani ya mwezi huo akiwa na takwimu nzuri kuwazidi makocha wote.

Raia huyo wa Ufaransa ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na timu yetu Aprili mwaka huu.

Kwa upande wa Chama tuzo yake imepokelewa na Meneja wa Timu, Patrick Rweyemamu kutokana na kiungo huyo kuwa nchini Zambia akihidhuria msiba wa mkewe aliyefariki dunia leo.

Katika mwezi huo Chama amefunga mabao matatu na kusaidia kupatikana kwa mengine (assist) matano.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. #Mungu awe upande wetu daima kulingana na juhudi zetu tunazozifanyaa akatupe ubunifu na maarifa zaidii ya kufanikisha mpira wetu @Tanzania
    Thanks @Simba nguvu moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER