Gomes, Bocco wang’ara tuzo za VPL Juni

Kocha Didier Gomes amechaguliwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa mwezi Juni huku Nahodha John Bocco akichaguliwa mchezaji bora.

Gomes ametuwezesha kushinda mechi zote tatu tulizocheza Juni ambazo zilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Polisi Tanzania, na Mbeya City.

Gomes raia wa Ufaransa amewashinda Nasreedine Al Nabi wa Yanga na George Lwandamina wa Azam ambao aliingia nao fainali.

Hii ni mara ya pili kwa Gomes kuchukua tuzo ya kocha bora wa mwezi baada ya kufanya hivyo Aprili kwa mara ya kwanza.

Kwa upande wake Bocco amefunga mabao matatu ndani ya mwezi Juni na kuwashinda Feisal Salum wa Yanga na Idd Seleman ‘Nado’ wa Azam.

Bocco nae ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER