Gomes awataja wachezaji mafanikio ya Simba 2020/21

Kocha Mkuu Didier Gomes, amesema mafanikio tuliyopata msimu wa 2020/21 yamechangiwa kiasi kikubwa na umahiri wa wachezaji wetu.

Gomes amesema kutetea ubingwa wa Ligi Kuu, Azam Sports Federation Cup na kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kumetokana na ubora wa kikosi tulicho nacho.

Licha ya ubora wa kikosi Gomes ameupongeza uongozi wa klabu chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez kwa kumpa ushirikiano mkubwa na kufanya mazingira ya kazi yake  kuwa mepesi.

“Msimu huu tumekuwa na kikosi bora na tumestahili kushinda taji la ligi na lile la Azam Sports, najivunia sana kufanya kazi na wachezaji hawa walifanya kila kitu kuhakikisha tunafikia malengo yetu.

“Pia uongozi ulinipa ushirikiano mkubwa nilipata kila nililohitaji kwa wakati na kufanya mazingira ya kazi yangu kuwa mepesi,” amesema Gomes.

Gomes tayari amesafiri kuelekea nchini kwao Ufaransa kwa mapumziko ya siku 10 kabla ya kurejea kuanza maandalizi ya msimu mpya wa 202/22, Agosti 8, mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Mimi ni mshabiki wa Simba damu damu, nakupenda Sana Simba. Ushauri wangu ni kwamba naomba viongozi waendelee na Moyo wao wa dhati na utendeji. Pia nakuomba uongozi wa Simba pale wanapotaka kusajili Basi waangalie wachezaji wazuri Insha’Allah tutachukua ubingwa wa Afrika. Ombi langu binafsi naomba nafasi ya kazi katika klabu ya Simba. Nawatakia kazi njema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER