Gomes awataja Mo, Barbara, wachezaji ubingwa VPL

Kocha Mkuu Didier Gomes, amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji (Mo) na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kwa ushirikiano waliompa hadi kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jana.

Gomes amesema uongozi wa klabu ukiongozwa na Mo na Barbara wamemuamini na kumpa ushirikiano mkubwa na ndiyo sababu iliyotufanya kutwaa ubingwa tukiwa na mechi mbili mkononi.

Gomes amesema huwezi kuwa kocha bora bila kuwa na wachezaji bora hivyo amekimwagia sifa kikosi chetu kwa uimara wake huku akisema tumestahili kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Raia huyo wa Ufaransa amesema msimu huu tumekuwa bora na tumestahili kutwaa ubingwa kwa sababu ndiyo timu iliyofunga mabao mengi na kufungwa machache kuliko zote.

“Lazima tumshukuru Mwenyekiti wa Bodi na CEO Barbara kwa ushirikiano walionipa kwanza kuniamini naweza kuifundisha hii timu na kuipa mafanikio.

“Pia siwezi kuacha kuwataja wachezaji wangu kwenye ubingwa huu, huwezi kuwa kocha bora bila kuwa na wachezaji bora pia tulikuwa na kikosi imara. Tumestahili kuwa mabingwa msimu tulikuwa bora zaidi ya timu zote,” amesema Gomes.

Hadi sasa tumebakisha mechi tatu kukamilisha msimu wa Ligi 2020/21, michezo miwili ikiwa ya ligi na fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup itakayopigwa Julai 25, mkoani Kigoma.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. KUTOKA URAMBO TABORA TNZANIA,,,,,Kila mwana msimbazi anafurahiya matokeo yake yanakua yakuwavutia binafsi nakupenda mchezo wa Simba na uongozi wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER