Gomes afanya Mabadiliko kikosi cha kuikabili Coastal

Kocha Didier Gomes amefanya mabadiliko ya wachezaji watano kwenye kikosi cha kwanza ambacho kitashuka dimbani kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mlinda mlango Beno Kakolanya ameanza kuchukua nafasi ya Aishi Manula wakati David Kameta akichukua nafasi ya Shomari Kapombe upande wa ulinzi wa kulia.

Gadiel Michael amepangwa kucheza mlinzi wa kushoto akichukua nafasi ya Mohamed Hussein wakati Ibrahim Ame na Kennedy Juma wakichukua nafasi za Pascal Wawa na Joash Onyango.

Erasto Nyoni amepangwa kucheza nafasi ya kiungo wa ulinzi ambapo mara kadhaa Taddeo Lwanga amekuwa akicheza.

Nahodha John Bocco na Chris Mugalu wataongoza mashambulizi wakisaidiwa na Luis Miquissone, Clatous Chama na Rally Bwalya.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), David Kameta (27), Gadiel Michael (2), Ibrahim Ame (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Clatous Chama (17), Rally Bwalya (8), John Bocco (22), Chris Mugalu (7),  Luis Miquissone (11).

Wachezaji wa Akiba: Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mzamiru Yassin (19), Taddeo Lwanga (4), Said Ndemla (13), Medie Kagere (14),Hassan Dilunga (24).

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER