Goli la mama larejea AFL

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa amesema Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ataendelea kutoa pesa ‘goli la mama’ kwa ajili ya hamasa kwenye michuano ya kimataifa na litaanza kutumika Ijumaa kwenye mchezo wetu wa ufunguzi dhidi ya Al Ahly.

Gerson ameyasema hayo Mbagala wakati wa zoezi la hamasa kuelekea mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL) ambayo leo tumeingia siku ya tatu.

Gerson amesema Rais Samia atatoa Shilingi 10,000,000 kwa kila bao tutakalofunga siku ya Ijumaa dhidi ya Al Ahly.

“Kama ilivyokuwa pochi la mama litaendelea katika michuano hii na tutaanza Ijumaa kila goli litajalofungwa Rais Samia atatoa Shilingi milioni 10,” amesema Gerson.

Gerson amesema Serikali ipo pamoja na klabu yetu katika maandalizi yote ya mchezo ndani na nje ndio maana tumetoka Dodoma tumekuja Dar es Salaam kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika kwa asilimia 100 kila kitu kipo sawa, tumekuja Dar es Salaam kuhakikisha kila kitu sawa na nikitoka hapa naelekea kambini kuonana na wachezaji,” amesema Msigwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER