Fatema Dewji afunguka mipango Simba Queens 2020/21

Mlezi wa Timu ya Simba Queens, Fatema Dewji ameweka wazi malengo yao msimu huu kuwa ni kutetea taji la Ligi ya Wanawake kwa mara ya pili mfululizo.

Fatema amesema wamewajenga wachezaji kisaikolojia na kimazoezi ili kutimiza azma hiyo ingawa anajua haitakuwa rahisi.

Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, Fatema amesema kila kitu kuhusu wachezaji kiko sawa na wana imani kubwa ya kupata ushindi.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatetea taji letu kwa mara ya pili mfululizo, kuelekea mechi ya kesho kila kitu kimekamilika na tunaamini tutapata matokeo ya ushindi,” amesema Fatema.

Kwa upande wake Msemaji wa timu hiyo, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti huku akiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi.

“Kwanza tunaelekea kwenye kilele cha siku ya Wanawake tunawaomba wanawake na Wanasimba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu na kitu pekee cha kuwahakikishia ni kuwa Yanga watalala mapema kesho,” amesema Monalisa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. mimi ni kijana mdogo wa kike mwenye uwezo wa kucheza mpira wa miguu, nina umri wa miaka 19 na nina ishi arusha. Nnaomba support ya timu ya simba queens niweze kuonyesha uwezo wangu kwa maana naamini nna uwezo mkubwa. Naombeni mnisaidie niweze kutimiza ndoto zangu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER