Kocha Mkuu Fadlu Davids na kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua wamekabidhiwa tuzo za Ligi Kuu ya NBC walizoshinda mwezi Agosti.
Wawili hao wamekabidhiwa tuzo zao kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.
Fadlu amewapiku, Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Mohamed Abdallah wa Mashujaa ambao aliingia nao kwenye kinyang’anyiro.
Kwa upande wake Ahoua amechaguliwa mchezaji bora baada ya kufunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu (Assist’) katika mechi mbili tulizocheza mwezi Agosti.