Fabrice Ngoma ni Mnyama

Ni rasmi tumefanikiwa kumsajili kiungo Fabrice Luamba Ngoma raia wa DR Congo kutoka Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa miaka miwili.

Ngoma ni mchezaji mzoefu ambaye anaweza kucheza kama kiungo mkabaji huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi kwa usahihi kutoka nyuma hadi mbele kwa washambuliaji.

Ngoma ni mchezaji mwenye wasifu mkubwa katika soka la Afrika na tunategemea ataongeza kitu kikubwa kwenye kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa mashindano 2023/24.

Ngoma anakumbukwa kwa kiwango bora alichoonyesha mwaka 2018 akiwa katika kikosi bora cha AS Vita kilichocheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca huku akifunga bao la tatu.

Mbali na Al Hilal na AS Vita, Ngoma ambaye ana urefu wa futi sita pia amewahi kuzitumikia klabu za Raja Casablanca (Morocco), Al Fahaheel FC (Kuwait) na Ifeanyi Ubah FC (Nigeria).

Ngoma atasafiri pamoja na wachezaji wengine waliokuwa wamebaki kuelekea nchini Uturuki kujiunga na wenzao wanaoendelea na kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER