Benki ya Equity imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Simba Bankers Bonanza baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya NBC katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Equity ambayo ilikuwa kundi A pamoja na Amana Bank, Stanbic na NBC ilionyesha tangu mwanzo kuwa imedhaamiria kutwaa ubingwa msimu huu kutokana na kiwango ilichokionyesha kwenye kila mchezo.
Katika mchezo wa fainali timu zote zikishambuliana kwa zamu huku NBC nao wakitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini walishindwa kuzitumia.
Mabingwa Equity wametapata medali za Dhahabu, Kombe, seti ya jezi ya Simba tunazotumia kwenye michuano Kombe la Shirikisho Afrika na tiketi za mchezo wa Jumatano dhidi ya Al Masry.