Emirate yamfanyia ‘surprise’ Ahmed Ally

Kampuni ya Emirate Aluminium ACP imemshtukiza Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally kwa kumkabidhi kitita cha Sh 2,000,000 baada ya kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha mashabiki mwezi Aprili.

Tukio hilo limetokea katika Ofisi za Emirate Aluminium ACP zilizopo Sinza Madukani muda mfupi baada ya mlinzi wa kati Henock Inonga kukabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili.

Meneja Mahusiano wa Emirate Aluminium ACP, Issa Maeda amesema kampuni hiyo imetambua mchango wa Ahmed wa kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani hasa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kampuni ya Emirate Aluminium inatambua mchango wa Ahmed Ally kwa hamasa kubwa aliyofanya kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na tumemkabidhi fedha taslimu Sh 2,000,000 kama zawadi yetu kwake kwa kazi nzuri aliyoifanya,” amesema Maeda.

Baada ya kukabidhiwa kitita hicho Ahmed amewashukuru Emirate kwa kutambua mchango wake huku akiweka wazi si chake peke yake bali Kitengo kizima cha Habari na Mawasiliano.

“Nawashukuru sana Emirate kwa zawadi hii lakini hii si kwa ajili yangu pekee bali kitengo kizima cha habari pamoja na waandishi wote tulioshirikiana wakati wa kampeni nzima. Nitagawa sehemu kwa ajili ya wenzangu,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER