Emirate Aluminium yatia mkono mechi, Simba, Kaizer Chiefs

Kampuni ya Emirate Aluminium Profile itatoa Sh 5,000,000 kwa mchezaji bora wa mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa Jumamosi Mei 15 katika Uwanja wa FNB jijini Johannesburg na ule wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zitolewa mara mbili yaani 2,500,000 katika kila mchezo.

Emirate Aluminium ambao pia ni wanadhamini wa tuzo ya mchezaji bora wa kila mwezi wa mashabiki (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) watatoa fedha hizo ili kuongeza ari kwa wachezaji kupambana kuwezesha timu kupata ushindi.

Afisa Uhusiano wa Emirate Aluminium, Issa Maeda amesema lengo lao ni kuchangia kuongeza hamasa kwa wachezaji ili kuhakikisha Simba inafuzu na kuingia nusu fainali ya michuano hiyo.

“Tutatoa Sh 2,500,000 kwa mchezaji bora wa mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs na pia tutatoa kiasi kama hicho katika mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam, Mei 21 lengo ni kuongeza ari kwa wachezaji,” amesema Maeda.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. Mshabiki kutoka visiwani Zanzibarkatika kijiji cha Jambiani. Hongera sana Simba kwa kutupa burudani nafsi inappenda.

    Lakini pia na taarifa zaSimba Queens mutupatie.

    Ahsane sana
    Mbarak

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER