Nyota wetu mpya Duncan Nyoni ameanza mazoezi rasmi na wachezaji wenzake hapa kambini nchini Morocco.
Duncan raia wa Malawi amejiunga leo kambini na moja kwa moja ameanza kujifua tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22.
Usajili wa Duncan ulikamilika siku nne zilizopita akitokea Silver Strikers FC ya nchini kwao kabla ya kusafiri hadi huku Morocco kujiunga na wenzake.
Duncan ameungana na nyota wengine wa kigeni tuliowasajili msimu huu kama Peter Banda, Henock Inonga na Pape Ousmane Sakho.
Kikosi chetu kimeanza mazoezi ya maandalizi hapa Morocco, Agosti 12 na kitakuwa huku kwa siku 20 kabla ya kurejea nchini.
One Response
Simba oyeeeeeee