Duchu arejeshwa tena Unyamani

Mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kusalia katika kikosi chetu.

Duchu tulimsajili kutoka Lipuli FC, Julai 2020 akatumikia msimu mmoja kabla ya kumtoa kwa mkopo katika timu za Biashara United, Geita Gold na Mtibwa Sugar.

Kiwango cha Duchu kimeimarika na benchi la ufundi limeona ni muda muafaka wa kurejea kikosini kuitumikia timu kuelekea msimu wa ligi 2023/24.

Kurejea kwa Duchu kikosini ni kama usajili mpya sababu tulimkosa kwenye kikosi chetu kwa miaka miwili.

Duchu atakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER