Droo ya Simba University Bonanza yakamilika Crown Media

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally ameongoza zoezi la upangaji wa Droo la Simba University Bonanza ambalo litakutanisha wanachuo kutoka vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam likilofanyika katika Studio za Crown Media.

Bonanza hilo ambalo lengo lake ni kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili katika mchezo wetu wa tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien.

Bonanza hilo ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Yas pamoja na Chuo cha City College litahusisha vyuo 14 ambapo kutapigwa mechi saba na kila atayeshinda ataingia hatua inayofuata.

Hii hapa droo kamili ya makundi iliyopangwa

1. TIA Simba Fans VS Kampala University

2. Bandari College VS Ustawi wa Jamii

3. Wakali wa DIT VS ST. Joseph Afya

4. Wekundu wa Posta IFM VS CBE Simba Fans

5. DSJ VS Tumaini University

6. Utumishi wa Umma vs UDSM

7. City College VS ST. Joseph Mbezi

Katika Bonanza la kesho kutakuwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini pamoja na vikundi mbalimbali vya mashabiki ili kuongeza chachu ya ushindani.

Mdhamini City College atatoa zawadi ya tiketi 30 kwa Mabingwa kwa ajili ya mchezo wa Jumapili huku pia kukiwa na zawadi ya mchezaji bora wa kila mechi, Mchezaji bora wa mashindano, Golikipa bora na beki bora.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER