Daktari wa timu, Yassin Gembe amewatoa hofu wapenzi na mashabiki kuhusu hali ya kiafya ya mlinda mlango namba moja Aishi Manula kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata majeraha jana.
Manula alitolewa dakika ya 65 baada ya kugongana na mshambuliaji wa JKT Tanzania, Danny Lyanga na kupelekea kupoteza fahamu na kukimbizwa Hospitali ambapo alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri.
Dk. Gembe amesema Manula anaendelea vizuri hakupata jeraha kubwa ingawa wanasubiri vipimo zaidi kujua hali yake na anataraji kuwepo kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Merreikh.
“Manula anaendelea vizuri jana aliumia kichwani lakini anaendelea vizuri tunasubiri vipimo zaidi na hakuna jambo la kuhofia zaidi,” amesema Dk. Gembe.
3 Responses
get well soon #airmanula 🦁 #nguvumoja💪
Alhamdulilah
Atakuwa sawa. Tuko nyuma yenu viongozi wetu
Tunamuombea kila la kheri na Mungu awe pamoja naye golikipa wetu mpendwa