Dilunga akabidhiwa tuzo yake na Emirate Aluminium ACP

Kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga, amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa Oktoba wa mashabiki (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) na wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Dilunga amewapiku viungo wenzake Rally Bwalya na Sadio Kanoute ambao waliingia fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Emirate imemkabidhi kitita cha Sh 2,000,000 na ngao kama sehemu ya zawadi baada ya kunyakua tuzo hiyo.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Emirate Aluminium ACP, Issa Maeda amesema ni tuzo kubwa ambayo inatolewa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati na haijawahi kutolewa kabla.

“Emirate Aluminium ACP tunatoa kiasi kikubwa cha fedha kwa mchezaji bora wa Simba, ni kikubwa mara mbili zaidi ya msimu uliopita, hata mchezaji bora wa ligi hapati kama hiki nadhani itaongeza chachu kwa wachezaji kuendelea kufanya vizuri,” amesema Maeda.

Kwa upande wake Dilunga amewashukuru mashabiki kwa kumpigia kura nyingi na wamemfanya kujiona ana deni kubwa na ataendelea kujituma kama sehemu ya kurejesha shukrani kwao.

“Kwanza nawashukuru mashabiki kwa kunipigia kura nyingi, naishukuru familia yangu na marafiki wa karibu kwa kuhamasisha mpaka nikapata tuzo hii, kiukweli najiona nina deni kubwa na nitaendelea kupambana kupata tena na tena,” amesema Dilunga.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa.

Dilunga kura 2249
Bwalya kura 2199
Kanoute kura 376

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER