Derby ya Mzizima haina mbabe

Mchezo wa Derby ya Mzizima uliopigwa Uwanja wa Azam Complex kati yetu na Azam FC umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Rogers Kola aliwapatia Azam bao la kwanza dakika ya 37 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Lusajo Mwaikenda.

John Bocco alitusawazishia bao hilo kwa kichwa dakika ya 45 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na Shomari Kapombe.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika 20 za mwanzo Azam walimiliki sehemu kubwa ya mchezo wakifika zaidi langoni kwetu.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Kibu Denis, Rally Bwalya na Bocco na kuwaingiza Peter Banda, Yusuf Mhilu na Medie Kagere.

Sare ya leo inatufanya kufikisha pointi 50 alama 10 nyuma ya vinara baada ya kucheza mechi 24.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER