Dejan Kuongoza mashambulizi dhidi ya Malindi leo

Mshambuliaji Dejan Georgijevic amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Malindi FC utakaopigwa Uwanja wa Amani saa 2:15 usiku.

Mara kadhaa Dejan amekuwa akipangwa kutokea benchi lakini leo kocha Juma Mgunda ameamua kumuanzisha kuongoza mashambulizi.

Dejan atasaidiwa na viungo washambuliaji Augustine Okrah, Nelson Okwa na Peter Banda.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Augustine Okrah (27), Nassor Kapama (35), Dejan Georgijevic (7), Nelson Okwa (8), Peter Banda (11).

Wachezaji wa Akiba

Ahmed Feruz (31), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Victor Akpan (6), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Jimmyson Mwanuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER