Dejan kuongoza mashambulizi dhidi ya Al Hilal leo

Mshambuaji Dejan Georgijevic amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo dhidi ya wenyeji Al Hilal katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan.

Mara zote tangu ajiunge na kikosi chetu Dejan amekuwa akitokea benchi lakini leo Kocha Zoran Maki na benchi lake wameona anatakiwa kuongoza mashambulizi.

Dejan atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Pape Sakho na Peter Banda.

Israel Patrick ambaye mara zote anacheza mlinzi wa kulia leo amepangwa kucheza kiungo mkabaji akisaidiana na Augustine Okrah.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Ally Salim (1), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Nassor Kapama (35), Henock Inonga (29), Israel Patrick (5), Pape Sakho (10), Augustine Okrah (27), Dejan Georgijevic (7), Clatous Chama (17), Peter Banda (11).

Wachezaji wa Akiba

Ahmed Feruzi (31), Nelson Okwa (8), Moses Phiri (25).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER