Debora Fernandes ni Mnyama

Kiungo ‘fundi’ Debora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Congo Brazaville lakini anaechezea timu ya taifa ya Gabon amejiunga nasi kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Mutondo Stars ya Zambia.

Debora anamudu pia kucheza kama kiungo mkabaji namba sita ingawa anafurahi zaidi kucheza juu kidogo yaani namba nane.

Ujio wa Debora unaongeza nguvu katika eneo letu la kiungo kwakuwa anaweza kuzuia na kupiga pasi sahihi kuelekea mbele na kuanzisha mashambulizi.

Tunaendelea kusuka timu imara kwa ajili muda mrefu ndio maana usajili wetu umezingatia umri wa wachezaji tunaowasajili.

Debora anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa katika idara ya kiungo wa kati baada ya jana kumsajili Augustine Okajepha lengo likiwa ni kuongeza uimara wa kikosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER