Daniel Cadena Kocha wetu mpya wa makipa

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri Daniel Cadena kuwa kocha wa makipa wa kikosi chetu kwa mkataba wa miaka miwili.

Cadena (45) raia wa Hispania ana leseni ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) na uzoefu wake ni mkubwa.

Cadena ana wasifu mkubwa ambapo amezifundisha timu mbalimbali barani Ulaya, China pamoja na Falme za Kiarabu kabla ya kuja Afrika.

Cadena amejiunga nasi akitokea Azam FC alipodumu kwa mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Cadena amewahi kukinoa kikosi cha timu ya vijana Sevilla FC ya Hispania msimu wa 2018-2019.

Cadena anachukua nafasi ya Chlouha Zakaria raia wa Morocco ambaye tumeachana naye mwezi uliopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER