Damons kocha mpya wa makipa

Klabu yetu imemtangaza Kocha Mpya wa Makipa, Tyron Damons raia wa Afrika Kusini (43) akichukua nafasi ya Milton Nionov ambaye mkataba wake ulisitishwa miezi miwili iliyopita.

Kocha Damons ana Diploma C na D ya Shirikisho la Soka Barani Afrika pia ameshiriki kozi mbalimbali za ukipa kama KVBN, SAFA na Evolution Conference iliyofanyika nchini Uingereza.

Kabla ya kujiunga nasi alikuwa kocha wa makipa wa Chipa United inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Pia Damons amezifundisha timu nyingine nchini Afrika Kusini kama TS Galaxy msimu wa 2018/19 na Bidvest Wits msimu wa 2016/19.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER