CRDB yaidhamini Simba Day

Benki ya CRDB imeingia ushirika na klabu yetu kudhamini Tamasha letu la Simba Day litakalofanyika Agosti 8, mwaka huu ambapo wameweka Sh milioni 25.

Fedha hizo zitatumika katika maandalizi na sherehe hiyo ambayo mwaka huu itakuwa kubwa na tofauti kutokana na jinsi inavyoratibiwa.

Mtendaji Mkuu wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki hiyo imekuwa ikijihusisha na michezo na msimu huu wameamua kuwa sehemu ya tamasha hili lenye historia kubwa.

“Benki ya CRDB tumeamua kuwa sehemu ya Tamasha la Simba Day kwa kuwawezesha kiasi cha Sh 25 kwa ajili ya maandalizi. Simba ni timu kubwa na hata sisi wafanyakazi wetu asilimia 50 ni mashabiki wa Simba, tunaamini huu ni mwanzo mzuri kuendeleza uhusiano mzuri baina yetu,” amesema Nsekela.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez amesema CRDB imeongeza thamani ya Simba Day na kadiri muda unavyozidi kwenda linakua zaidi.

“Benki ya CRDB ni mshirika rasmi wa Simba Day tunawashukuru kwa kuiongezea thamani siku hii muhimu na kuifanya iwe kubwa zaidi,” amesema Barbara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER