Corazone, Rufa wang’ara Tuzo Ngao ya Jamii

Kiungo mkabaji, Vivian Corazone amechaguliwa mchezaji bora wa mashindano ya Ngao ya Jamii na mlinda mlango Carolyene Rufa akiibuka golikipa bora wa michuano.

Corazone mbali na mchango mkubwa aliokuwa anautoa kwenye kikosi pia amefunga penati za mwisho zilizotoa maamuzi katika mechi zote mbili.

Kwa upande wake Rufa amechaguliwa mlinda mlango bora baada ya kuonyesha kiwango bora katika mechi ya kwanza dhidi ya Yanga Princess na leo ameokoa penati ya mwisho iliyotupa ubingwa wa Ngao ya Jamii.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER