Che Malone ni Mnyama

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumsajili mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone (24) raia wa Cameroon kutoka Cotton Sports FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Che Malone amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Cotton Sports kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Cameroon msimu uliopita akiwa nahodha huku akicheza karibia mechi zote.

Che Malone ambaye anajulika kwa jina la utani ‘Ukuta wa Yericko’ ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Cameroon (MVP) msimu wa 2022/23.

Che Malone ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon ‘Indomitable Lions’ pamoja na timu inayoshiriki michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Che Malone ni mchezaji mwenye uzoefu wa kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Shirikisho hivyo tunaamini atakuwa msaada mkubwa kikosini.

Che Malone anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga nasi katika dirisha hili la usajili baada ya Willy Essomba Onana na Aubin Kramo Kouame.

Uongozi wa klabu unaendelea kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya wa ligi 2023/24 na lengo letu ni kuhakikisha tunarejesha mataji yetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER