Che Malone: Najisikia fahari kuwa sehemu ya Simba

Mlinzi wa kati Che Fondoh Malone amesema anajisikia fahari kuwa sehemu ya kikosi kitakachoiwakilisha timu yetu kwenye msimu mpya wa mashindano 2023/24.

Che Malone ambaye tumemsajili kutoka Cotton Sports ya Cameroon amesema Simba ni moja ya timu kubwa Afrika hivyo kila mchezaji angependa kuitumikia.

Akizungumzia Simba Day ya kesho, Malone amesema itakuwa siku kubwa kwakuwa mashabiki watapata nafasi ya kuiona timu yao kwa mara ya kwanza pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa.

“Kesho ni siku kubwa, tunajua mashabiki wana hamu ya kuiona timu yao. Wanataka waone timu inachezaje pamoja na wachezaji wapya, nafurahi kuwa sehemu ya kikosi.

“Binafsi sina hofu ya wingi wa mashabiki watakaojitokeza kwa wingi uwanjani kesho, nimejipanga kuhakikisha ninafanya vizuri kama nitapata nafasi ya kucheza,” amesema Che Malone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER