Baada ya kufanya mazoezi ya Gym asubuhi nyota wanne Che Fondoh Malone, Jean Baleke na Aubin Kramo Kouame wamefanya mazoezi ya uwanjani jioni.
Asubuhi walifanya mazoezi ya gym ili kuweka miwili yao sawa lakini jioni wamefanya mazoezi ya uwanjani.
Hata hivyo nyota hao wamefanya mazoezi ya peke yao sababu wamechelewa kufika kambini hivyo wanapaswa kuwa fiti ili kuenda sawa na wenzao.
Wachezaji wengine wameendelea na mazoezi kama kawaida kwa mujibu wa programu ilivyopangwa.