Chama: Tuko tayari kwa Ruvu Shooting

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amesema wachezaji wote wamejipanga tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora wa Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) utapigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Chama amesema wachezaji wana ari ya hali ya juu na kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo akitambua lengo ni kushinda na kufuzu robo fainali.

Chama ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na Ruvu Shooting mara zote wamekuwa wakitusumbua lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Kwa upande wetu wachezaji tuko kamili, tuko tayari kutimiza maagizo tutakayopewa na benchi la ufundi na kila atakayepata nafasi atakuwa atapeperusha vema bendera ya Simba,” amesema Chama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER