Chama, Sakho, Kanoute kuchuana Mchezaji Bora Agosti

Nyota wetu watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kutafuta Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month) wa mwezi Agosti.

Nyota hao ambao wamekuwa na takwimu nzuri kutokana na kufanya vizuri ni viungo Clatous Chama, Pape Sakho na Sadio Kanoute.

Wachezaji wawili ambao tumewasajili msimu huu mlinzi wa kati Mohamed Ouattara na kiungo mshambuaji Augustine Okrah waliingia kwenye tano bora kutokana na ubora walioonyesha.

Takwimu za wachezaji wote Mechi Dakika Goli Assist

Chama 3 231 1 3

Sakho 3 256 1 0

Kanoute 3 239 0 0

Zoezi la kupiga kura zitaanza leo saa 11 jioni hadi Septemba Mosi saa sita usiku kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz

Mshindi wa jumla atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER