Chama Mchezaji bora wa mashabiki Machi

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Chama amewashinda mlinda mlango, Aishi Manula na mshambuliaji Jean Baleke ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Machi, Chama amecheza mechi nne sawa na dakika 273 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa jingine moja.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia
Chama 853 53.8%
Manula 383 24.2%
Baleke 348 21.9%

Hii ni mara ya tatu msimu huu Chama anachaguliwa mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki ambapo amefanya Agosti, Desemba na Machi.

Chama atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER