Chama Mchezaji Bora wa Mashabiki Agosti

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Agosti (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Chama amewashinda viungo wenzake Pape Sakho na Sadio Kanoute ambao aliingia nao fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.

Chama ameshinda kutokana na kupata kura nyingi kutoka kwa mashabiki zilizopigwa kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz kuanzia Agosti 29 hadi Septemba Mosi.

Kwa ushindi huo Chama atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa

Kura Asilimia Nafasi

Chama 1551 60.30 1

Sakho 506 19.63 3

Kanoute 516 20.06 2

Katika mwezi Agosti Chama amecheza mechi zote tatu sawa na dakika 231 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Simba always have a great moment, and we’re always looking for our duty 💪💪💪hivo tupambane pamoja kwa kila hatua yetu, shout-out for the simbaaaaaaa akee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER